Picha: Sitti Mtemvu ashinda taji la Miss Temeke 2014, angalia picha zaidi

Shindano la kumtafuta mrembo wa Temeke, Miss Temeke 2014 yalifanyika jana usiku katika ukumbi wa TCC Chang’ombe, jijini Dar es Salaam ambapo Sitti Mtemvu aliibuka mshindi.

Sitti Mtemvu, Miss Temeke 2014
Sitti Mtemvu alilivaa taji hilo na kuwa mshindi wa kwanza huku mrembo Salama Saleh akishika nafasi pili, na Neema Mollely alitajwa kuwa mshindi wa tatu.
Matokeo hayo yanawapa warembo hao watatu  tiketi ya kuwa wawakilishi wa Wilaya ya Temeke katika mashindano ya kumtafuta mrembo wa Tanzania (Miss Tanzania 2014).
Shindano hilo lililokuwa na washiriki 17 lilishereheshwa na Gardener G. Habash, mtangazaji wa kipindi cha Maskani cha 100.5 Times Fm lilipambwa na burudani toka kwa wasanii mbalimbali akiwemo TID na Young Suma.


Gardener G Habash akiwa na Abdalah Gunda wa kitengo cha masoko cha Airtel
Meza ya Majaji


Picha: Sitti Mtemvu ashinda taji la Miss Temeke 2014, angalia picha zaidi Picha: Sitti Mtemvu ashinda taji la Miss Temeke 2014, angalia picha zaidi Reviewed by Unknown on 12:07:00 Rating: 5
Powered by Blogger.