PADRI ALIYERUHUSUWA KUOA TANZANIA

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa
Francis amekubali kumuondolea sakramenti ya upadri, Raymond Mosha wa
Jimbo Katoliki la Moshi ikiwa ni miaka 20 tangu padri huyo aombe
kuachana na daraja hilo.
Barua ya uamuzi wa Papa Francis ilisomwa juzi
katika parokia na vigango vyote vya Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi
katika ibada zilizofanyika katika makanisa ya jimbo hilo.
Miongoni mwa parokia ambazo barua hiyo ilisomwa ni
Karanga ambako Paroko wake, John Matumaini alitoa tangazo hilo katika
ibada zote. Uamuzi huo ambao ni nadra kutolewa na Papa, unamaanisha kuwa
sasa padri huyo yuko huru kuoa na kuwa na familia.
Hata hivyo, wakati uamuzi huo ukitangazwa rasmi
juzi, tayari Padri Mosha ambaye ni profesa wa falsafa na maadili katika
Chuo Kikuu cha Nelson Mandela Arusha, ana mke na watoto watatu ambao kwa
sasa wako vyuo vikuu.
Padri Mosha alisema aliandika barua kuomba kuondolewa daraja hilo mwaka 1994 kabla ya uamuzi kutolewa juzi.
Katika orodha ya mapadre 185 wa Kanisa Katoliki
Jimbo la Moshi iliyopo katika tovuti ya jimbo hilo, jina la Padri Mosha
linaonekana likiwa ni namba 23.
PADRI ALIYERUHUSUWA KUOA TANZANIA
Reviewed by Unknown
on
06:20:00
Rating:
