Naombeni Msinilaumu kwa Uamuzi Huu Niliouchukua kwa Mume Wangu
Mimi
nimeolewa miaka 15 sasa na tumejaaliwa watoto 4. Ndoa yetu ilipofikisha
miaka 4-5 mume wangu alicheat, nikamkamata through sms akapinga sn
lakini baadae alikubali akakiri kosa na kuomba msamaha. nikamsamehe
Tumeendelea
kuishi na nilipopata mtoto wa tatu akanicheat tena, safari hii alikuwa
nje ya nchi kimasomo, napo alikiri na kuomba msamaha, nikamsamehe
wakati
niko mjamzito mimba ya mtoto wa nne alinicheat tena, kibaya zaidi
alinicheat na house girl wng akampa ujauzito. kwa ivo wkt mimi nina
mimba na House girl naye mjamzito(japo sikujua km house girl alikuwa
mjamzito kwani aliondoka nyumbani) niligundua baadae kuwa mtt wa
aliyekuwa house Girl wangu ni wa mume wangu
kama
kawaida yake akaomba msamaha safari hii hadi kupiga goti na kulia ili
nimsamehe...na mimi kwa kuwa bado nampenda na nimemvumilia kwa mengi
nikaamua kumsamehe tena..ila tulikubailana masharti mengi na akakubali
masharti yote niliyompa..mwanzoni alibehave vizuri sn akawa muwazi kwng
hanifichi chochote kuhusu huyo mtt.. na tuliishi maisha ya furaha kwn
alinijali mno na alionekana kweli amerigrate.
sasa
cha kushangaza siku za karibuni amebadilika san, amekuwa msiri na
hasemi chochote kuhusu huyo mtt wa nje..siku hizi anatuma hela kwa siri
na pia anawasiliana na huyo mama wa mtoto kwa siri haniambii chochote..
nikajaribu
tena siku nyingine kumuuliza na majibu ndio hayo hayo, kwa kifupi
hataki na anakwepa kuzungumzia hilo suala kabisa...sasa najiuliza kwa
nini anafanya siri? km hakuna jambo lolote baya basi anaficha nini? ina
maana kuna kitu zaidi ya mtoto.
Sasa jamani mimi nimeamua km ifuatavyo
1. Na
mimi nimeamua kuwa na mahusiano nje ya ndoa, jamani msinilaumu nami pia
nahitaji kuliwazwa na kufarijiwa kwa kifupi nimechoka na mastress
yasiykuwa na mwisho, sikuwahi kumcheat mume wng ktk maisha yote ya ndoa.
ila sasa atanisamehe tu ht akijua wl sijali, nipo tayari kwa lolote..
2. Sina
mpango wa kuondoka kwenye nyumba tuliyojenga pamoja nitaishi hapa hapa
kwani sipendi wtt wng walelwe na mzazi mmoja..wtt hawajui kinachoendelea
in fact hata ndugu na jamaa hawajui chochote kwani mimi sijawaambia na
wala sijawahi kuwaeleza matatizo ya ndoa yng..kwa nje tunaonekana
familia iliyobarikiwa na ina furaha lkn wenyewe ndio tunaojua ndani
kukoje
3.
Kwa sababu sisemagi matatizo yangu kwa ndugu na marafiki nimeamua
kuweka hapa labda nitapunguza kitu fulani kichwani kwani sometime naona
km nazidiwa mawazo vile
Naombeni Msinilaumu kwa Uamuzi Huu Niliouchukua kwa Mume Wangu
Reviewed by CapchaMuzic
on
04:44:00
Rating: