Nani Zaidi: Wema Sepetu VS Jokate Mwengelo

Wema Sepetu na jokate mwengelo ni kati ya wasichana warembo hapa bongo na role models. Wote mwanzo wao ulitokana na mashindano ya miss Tanzania ya mwaka 2006 ambapo wema sepetu aliibuka mshindi wa kwanza huku jokate akikamata namba mbili.
Wema_na_Jokate
Najua huwezi kumuongelea wema sepetu au jokate bila kumuingiza diamond platnumz kidogo. Mnamo mwaka 2010 hadi 2011 diamond alianza kwanza kumdate mshindi wa kwanza wa miss tz jokate na kuachana nae na kuamia kwa mshindi wa pili yaani wema. Je, diamond nae alikua anataka kujibu swali tunaloliuliza ?  na kama amelijibu inabidi kushare jibu ilo na mashabiki tukajue.
wema-jokate-dating-diamond-www-vibe-co-tz-website
Wema na jokate wote wanafanya movie na vigumu kujua nani zaidi katika uigizaji wa movie sababu kila mtu anasababu yake ya kumkubali mmoja wao.Twende kwenye fashion wema na jokate wamekua role models wa warembo wengi katika swala la uvaaji.
wema-jokate-fashion-www-vibe-co-tz-website
Tukija kwenye Ujasiriamali  wema na jokate hawapo nyuma. Wema alianzisha kampuni yake ya Endless Fame Films ambayo inatengeneza bongo movies. Pia wema anakipindi chake cha TV kinachoitwa In My Own Shoes kinachooneshwa na Channel 5 EATV. Tukija kwa Jokate mwengelo kikubwa kwake ni product ya Kidoti inayompa chati sana ukiachana na kazi ya utangazaji anayofanya kwenye channelO ya Afrika Kusini.
wema-jokate-products-www-vibe-co-tz-copyrighted
Hata vibe magazine tuliliona hilo na kuamua kuwaweka wema na jokate katika cover page wakati ndio kwanza kuna issue tatu tu huku nyingine ikiwa ni kijana aliyewahi kuwadate wote diamond platnumz.
vibe-magazine-wema-jokate
kuanzia u-miss , fashion , ujasiriamali , ushawishi na kila kitu , je nani zaidi ?
Nani Zaidi: Wema Sepetu VS Jokate Mwengelo Nani Zaidi: Wema Sepetu VS Jokate Mwengelo Reviewed by Unknown on 12:29:00 Rating: 5
Powered by Blogger.