MAMA AMCHANA MWANAWE WA MIEZI MIWILI NA VIWEMBE SEHEMU YA HAJA KUBWA BAADA YA MTOTO KUZALIWA AKIWA HANA SEHEMU HIYO MATATIZO YA MAISHA YATAJWA KUWA SABABU
ANGALIA PICHA MAMA AMCHANA MWANAWE WA MIEZI MIWILI NA VIWEMBE
MWANDISHI
NA MMILIKI WA KIJUKUU BLOG WILLIAM BUNDALA KUSHOTO AKIFANYA MAHOJIANO
NA ANASTAZIA NGILITU JUU YA MAISHA YAKE NA SAKATA HILO LA KUMCHANA MTOTO
WAKE.
MAHOJIANO YAKIENDELEA
TITI LA KUSHOTO LA ANASTAZIA NGILITU LINALOSUMBULIWA NA UVIMBE
HAPA NIKIFANYA MAHOJIANO NA MAMA IVAN ALIYETAJWA KUWA MSAADA MKUBWA KWA ANASTAZIA NGILITU KIPINDI CHOTE CHA MATATIZO.
BI
ANASTAZIA NGILITU AKIWA NA MWANAE AKIMNYONYESHA TITI MOJA SIKU ZOTE
HALI INAYOPELEKEA MAZIWA KUISHA NA KULAZIMIKA KUMNYWESHA MAJI NA CHAI
MTOTO WA MIEZI MIWILI.
HAPA NILIMUULIZA SWALI AMBALO LILIMTOA MACHOZI,NI KUHUSU WATOTO WAKE
WENGINE WAKO WAPI? ALILIA SANA KABALA YA KUJIBU HAJUI HATA KAMA WAKO HAI
AU LAA.
MAHOJIANO YAKIENDELEA.
MWONEKANO WA MASIKIO YAKE BAADA YA KUVUTWA HELENI NA MUMEWE WA KWANZA.
NI MAMA MWENYE AFYA KABISA,ILA MAISHA NA MATESO NDIYO YANAMFANYA AWE OMBAOMBA.
MWANZA
mtoto huyo kuzaliwa akiwa hana sehemu ya Haja kubwa.
Tukio
hilo limetokea hivi karibuni baada ya mama huyo aliyefahamika kwa jina
la Anastazia Ngilitu kumchana kwa wembe zaidi ya mara tatu ili kumsaidia
mwanae kupata haja kubwa kwa kile kilichodaiwa mtoto huyo kuzaliwa
akiwa hana sehemu
ya haja kubwa.
Akiongea
na Kijukuu Blog mama huyo mkazi wa Tabora aishie jiini mwanza kwa sasa
amesema kuwa alijifungua watoto mapacha watatu ndani ya Mtaro kisha
wawili kufariki alipofikswa Hospitali na kusalia mtoto mmoja aliyekutwa
na tatizo la
na sehemu ya haja kubwa.
Sambamba
na hayo mama huyo amesema kuwa sababu za kumchana na wembe mwanawe ni
baada ya kumuona mtoto wake anashindwa kupata haja kubwa hali
iliyopelekea tumbo kujuaa na kulia.
Ameongeza
kuwa wakati wa kujifungua mtoto huyo walimfanyia upasuaji katika
hospitali ya Bugando ila hali ya kuziba ilijirudia tena na kuamua
kumchana kwa
kutoakana na kutokuwa na uwezo wa kulipia gharama za upasuaji hospitali.
Katika
hatua nyingine Mama huyo amesema kuwa kwa sasa hali yake ya Maisha siyo
nzuri kwani watoto wake wanaishi kwa kunywa maji na kwamba hapo awali
alikuwa anafanya kazi ya kufua nguo kwenye nyumba za watu ila kwa sasa
hawezi
kutokana na kuwa na motto mdogo.
Sambamba
na hayo mama huyu anasema kuwa licha ya kuolewa na wanaume watatu kwa
wakati tofauti na kila mmoja kumnyanyasa kwa kumpiga na mwingine
kumdhurumu pesa zaidi amesikitishwa na kitendo cha Mume wake wa sasa
hivi kumtaka kufanya mapenzi ikiwa tumbo la uzazi halijakaza hali
anayotaja kumsababishia maumivu makali na kutokwa na damu nyingi baada
ya mumewe
kumpiga.
Kitendo
cha mama huyu kumchana mtoto wake kwa wembe kinatoakana na hofu ya
kwenda hospitali kwani anasema hana uwezo wa pesa kwani kwa sasa yeye
mwenyewe anasumbuliwa na uvimbe katika titi lake la kushoto na alipoenda
Hospitali ya SEKOTURE aliambiwa gharama za upasuaji ni shilingi elfu 30
na
alipokosa alirudi nyumbani na kuendelea kujitibu kwa dawa za kienyeji.
Kwa
upande wao baadhi ya kina majirani ambao wamekuwa wakimpa msaada mama
huyu mara kwa mara,Wameiambia KIJUKUU BLOG kuwa mama huyu ana maisha
magumu kwani mume wake humpiga na kumfukuza mara kwa mara hali
inayomfanya aishi kwa kuomba omba na wakati mwingine kulala na watoto
wake
bila kula.
Taarifa
za awali zinaonyesha kuwa mama huyu aliolewa na mume wa kwanza mkazi wa
eneo la maji moto mkoani Mara na waliachana baada ya kupigwa na
kuchomwa kisu tumboni ikiwa ni pamoja na kupigiliwa msumali wa nchi sita
katikati ya mkono
wake wa kushoto ikiwa ni sambamba na
kumvuta hereni akimwambia kuwa ni dalili za kuwa malaya hali
iliyomsababibishia masikio yake kuvimba.
Mume
wa pili aliyemuoa mama huyo inaelezwa kuwa yeye alimdhurumu kiwanja
walichouza milioni moja na laki saba kilichokuwa eneo la makaburi Bwiru
kisha
kuzichukua na kuaga kwenda kuzifanyia biashara.
Kuhusu
ndugu Bi Anastazia amesema kuwa wazazi wake wote wamefariki na kwamba
aliyebaki ni bibi yake ambaye naye anamtaja kuwa ni mchawi kwani wakati
alipoenda Tabora,bibi yake alimwambia ampe mkono wa mtoto ili usiku wa
manane
amuamshe kwa kumpiga nao kichwani ili aende kazini.
Anastazia
anasema kuwa kutokana na matatizo hayo aliwahi kushauriwa kumtupa mtoto
huyo eneo la vichakani soko la sabasaba,ushauri aliopewa na rafiki yake
mkazi wa Ilemela aliyemtaja kwa jina moja la Amina ambaye alimwambie
mtoto wako hatapona,Jambo ambalo yeye alikataa na kusema kuwa anaogopa
mkono wa Sheria.
Tatizo
linalomsumbua mama huyo kwa sasa ni chakula na matibabu kwa mwanaye na
yeye mwenyewe anayesumbuliwa na uvimbe katika titi la kushoto na
kuwaomba wasamalia wema kumsaidia ili aendelee na shughuli zake
aondokane na
kuombaomba.
NDUGU MSOMAJI KAMA UNATAKA KUMSAIDIA MAMA HUYU NA KUWASILIANA NAYE WASILIANA NA NAMI KWA NAMBA+255 767 942 570
CHANZO KIJUKUU BLOG
MAMA AMCHANA MWANAWE WA MIEZI MIWILI NA VIWEMBE SEHEMU YA HAJA KUBWA BAADA YA MTOTO KUZALIWA AKIWA HANA SEHEMU HIYO MATATIZO YA MAISHA YATAJWA KUWA SABABU
Reviewed by Unknown
on
05:16:00
Rating: