MAAJABU YA DUNIA: MKE WA MCHUNGAJI AJIFUNGUA HIRIZI BAADA YA UJAUZITO WA MIEZI 9 BAGAMOYO...!
Na Edson Mkisi Jr
Wazee wetu walishawahi kuneno kwamba; Ukishangaa ya Mussa utayaona ya filauni! Ndivyo unavyoweza kuanza kusema kuhusiana na tukio la kushangaza lililotokea Kijiji cha Udindila Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Mchungaji wa Kanisa la
EAGT aliyetambulika kwa jina la Boniface Onesmo alijikuta akibubujikwa na machozi mara baada ya kushuhudia mkewe Bi. Benta Boniface akijifungua hirizi baada ya kushika mimba kwa kipindi cha miezi saba na nusu!
Akizungumza na mtangazaji wa Kipindi cha Hatua Tatu cha 100.5 Times Fm, Edson Mkisi Jr, Mchungaji huyo alisema kabla ya kutokea kwa tukio hilo mkewe amekuwa na matatizo ya kuharibika kwa mimba za mara kwa mara na tangu kuhamia kwa eneo hilo la Udingila Bagamoyo mkewe huyo hajawahi kuzaa mtoto hata mmoja angawa amekuwa akishika mimba kila walipohitaji kuzaa.
“Kwa hakika Mungu ni mwema na sitaacha kuendelea kumsifu na kumuabudu,” alianza kueleza Mchungaji Onesmo.
“Zaidi ya mtoto huyu mmoja niliyemzaa kabla ya kuhamia hapa, hivi sasa kila ninapotaka kuzaa mtoto mimba za mke wangu zinaharibika na hadi muda huu mimba zaidi ya nne zimeshaharibika nah ii nyingine ndio amezaa hirizi!” Mchungaji Onesmo alisimulia.
Aliezeza kuwa siku ya tukio, mkewe kipenzi alianza kusikua uchungu tangu saa nne asubuhi na kadri muda ulivyozidi kwenda ndivyo uchungu ulipozidi kuongezeka.
“Hali iliendelea hivyo hadi saa nne usiku ambapo mkewe alihisi kabisa kupushi na mimi nilikuwa tayari kumsaidia lakini wakati anaendelea kupushi mkewangu akawa anatoa haja ndogo mara kwa mara na alitoa haja ndogo hadi ndoo nne ndogo zilijaa na kumwaga nje.
“Baada ya hapo aliendelea kusikia maumivu makali ya tumboni huku akihisi kuzaa lakini baadae aliposikia mtoto anakuja na mimi kujiweka tayari kumzalisha niliona kitu kinatoka kama mtoto kukivuta ikatoka hirisi ikiwa imefungwa kitambaa chenye rangi chekundu na nyeusi!” anasema.
Aidha, kwa upande wa mkewe, alisema kama siki hiyo kungekuwa na sumu ya panya angekunywa afe akapumzike.
Akizungumze huku akilia, mama Dotto (Benta), anasema siku ya tukio hilo roho yake ilinusa kaburi kama kama kungekuwa na hata mafuta ya taa kwenye kopo angekunywa ili afe.
“Nilimuuliza mume wangu mara kadhaa kama kwenye kopo kuna mafuta ya taa lakini aliniambia yote aliweka kwenye kandiri (taa ya chemli) na hata nilipoangalia tunapoweka sumu sikuiona….kwa hakika kama ningekiona kimoja wapo ningekunywa nife! Nimetesema sana,” anasema mama Dotto.
Mama Dotto alisema pamoja na changamoto zote anazokutana nazo Bagamoyo lakini hajafikiria wala hafikirii kwenda kwa mganga wa kienyeji.
“Siwezi kwenda kwa mganga wa kienyeji kwa sababu waganga ukienda wao huongeza tatizo kwa hiyo nitaendelea kumuomba Mungu hadi atakaposikia maombi yangu,” anasema huku akiangalia na mumewe pamoja na majirani waliofika kumjulia hali.
Akizungumza na Mkisi Jr, Mjumbe wa eneo hilo, Bw Hamza Adam, mbali na kuthibitisha kufahamu kutokea kwa tukio hilo, pia alibainisha kwamba mbali na tukio hilo ambalo hajawahi kukutana nalo tangu uhai wake, pia eneo hilo mifugo imekuwa ikifa hovyo bila kuwepo kwa ugonjwa wowote.
Kwa undani wa tukio hilo, usikose kusikiliza kipindi cha Hatua Tatu cha 100.5 Times fm, kupitia kipengele cha Habari Ndio Hii Jumatatu tarehe 25 na Jumanne tarehe 26/08/2014 kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa sita mchana.
MAAJABU YA DUNIA: MKE WA MCHUNGAJI AJIFUNGUA HIRIZI BAADA YA UJAUZITO WA MIEZI 9 BAGAMOYO...!
Reviewed by Unknown
on
01:22:00
Rating: