KUHUSU KUVUNJIKA KWA KUNDI LA VICHEKESHO LA "ORIJINO KOMEDI",MASANJA MKANDAMIZAJI AFUNGUKA
Baada
ya miaka kadhaa ya kutamba kwa kundi la vichekesho la Ze Komedi kisha
kudaiwa kusambaratika, mmoja wa memba wa kundi hilo, Emmanuel Mgaya ‘
Masanja Mkandamizaji’ ameibuka na kueleza kutokana na ishu nzima.
Masanja
ambaye pia ni mchungaji amefunguka na kueleza kila kitu kuhusiana na
ishu hiyo huku akikanusha vikali kuwepo kwa uvunjifu wa kundi hilo.
Akizungumza
na mwandishi wetu, Masanja alisema kuwa kundi hilo halijavunjika kama
ilivyoripotiwa na kudai kuwa litarejea kama kawaida kuanzia mwezi
Septemba mwaka huu na kuendelea kubamba kama ilivyozoeleka kipindi cha
nyuma na kufanikiwa kujizolea umaarufu wa kutosha nchini.
“Kikubwa
tu watu waachane na hizo tetesi Ze Komedi kwamba imevunjika, nasema
kwamba haijavunjika wala hatujasambaratika hata kidogo, tupo na
tutaendelea kuwepo. Rasmi tutaanza kazi Septemba mwaka huu,” alisema
Masanja.
KUHUSU KUVUNJIKA KWA KUNDI LA VICHEKESHO LA "ORIJINO KOMEDI",MASANJA MKANDAMIZAJI AFUNGUKA
Reviewed by Unknown
on
07:46:00
Rating: