JACK PATRICK AHUKUMIWA CHINA

BAADA ya kushikiliwa kwa takriban miezi tisa kwa kesi ya madawa ya kulevya ‘unga’, hatimaye Video Queen maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ amehukumiwa kifungo cha miaka 6 jela huku kukiwa na uwezekano wa kupunguziwa adhabu ikawa ndogo zaidi.
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Jack, modo huyo alihukumiwa Jumatatu iliyopita (Agosti 11, mwaka huu) kwenye Mahakama ya Macau huko Hong Kong ambapo hukumu hiyo ilitofautiana na adhabu nyingine za madawa nchini humo ambazo huwa hukumu yake ni kunyongwa hivyo ya Jack kuonekana nyepesiii! KWA NINI NYEPESI?
Kikimwaga data, chanzo hicho makini kilidai kwamba, hukumu hiyo ya Jack ni nyepesi ukilinganisha na hukumu nyingine za madawa ya kulevya zinazotolewa nchini China ambapo hakimu alitumia muda wa dakika 27 tu kuisoma.
Hukumu za madawa ya kulevya zinatofautiana nchini China. Kuna baadhi ya majimbo kama Beijing huwa wao ikithibitika umebeba madawa ya kulevya, unanyongwa lakini baadhi ya maeneo unafungwa miaka kadhaa. Miaka hutofautiana kulingana na sheria walizojiwekea
kilifunguka chanzo chetu.
Ilidaiwa kwamba, kwa mujibu wa hukumu hiyo aliyohukumiwa mrembo huyo, anaweza kupunguziwa muda wa kifungo kulingana na nidhamu atakayoionesha gerezani kama mahakama ilivyoelekeza.
Anaweza akapunguziwa kifungo kwa sababu hukumu imeeleza wazi kwamba anaweza kupunguziwa adhabu hiyo kama atatimiza masharti ya kinidhamu ambayo sheria za China zinamtaka atimize
kilisema chanzo hicho.
TUJIUNGE NA CHANZO
Amehukumiwa juzi Jumatatu, ametakiwa kwenda jela miaka sita, nilikuwa nikiwasiliana naye mara kwa mara lakini juzi hiyo ndiyo kanitumia taarifa kwamba amehukumiwa na kunieleza kwamba siku hiyo aliduwaa kwa muda maana hakuamini kama anaweza kuhukumiwa kwani alikaa muda mrefu bila kujua hatima yake
kilisema chanzo hicho kilicho karibu na Jack.

JACK AFURAHIA HUKUMU! Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa, baada ya hukumu hiyo kupitishwa, Jack alifurahia hususan kuwepo kwa kipengele cha uwezekano wa kupunguziwa kifungo kama atakidhi masharti aliyopewa na mahakama.
JACK PATRICK AHUKUMIWA CHINA JACK PATRICK AHUKUMIWA CHINA Reviewed by Unknown on 02:36:00 Rating: 5
Powered by Blogger.