Interview: meninah azungumzia kipindi chake cha tv, kilichotokea baada ya kuripotiwa anatoka na Diamond, muwewe mtarajiwa, rushwa ya ngono kwenye media na..
Katika mahojiano hayo aliyofanya na Josefly Muhozi, amezungumzia kuhusu kipindi chake kipya cha runinga kitakachoanza hivi karibuni. Amezungumzia pia kilichojiri baada ya kusambaa ripoti kuwa anatoka na Diamond Platinumz na anavyomchukulia Wema Sepetu.
Kuhusu Muziki wake, Meninah ambaye hivi sasa ameachia ‘Pipi ya Kijiti’ ameeleza ugumu na mipango alinayo katika kuvuka mipaka na kufanikiwa zaidi.
Kuhusu Mapenzi, mwimbaji huyo amemzungumzia mumewe mtarajiwa na mwimbaji wa kiume ambaye kwa ‘ndoto’ zake anaota angekuwa mpenzi wake ‘kokote uliko kama unanisikia, I Love You’...! Sikiliza hapo chini akimtaja na kumpa ujumbe.
Meninah ambaye anasomea uandishi wa habari na utangazaji, ameeleza anachokifahamu kuhusu uwepo wa rushwa ya ngono kwenye media kati ya baadhi ya watu wa media na wasanii wa kike na ushauri wake.
Interview: meninah azungumzia kipindi chake cha tv, kilichotokea baada ya kuripotiwa anatoka na Diamond, muwewe mtarajiwa, rushwa ya ngono kwenye media na..
Reviewed by Unknown
on
12:15:00
Rating: