Hussein Machozi afunguka jinsi alivyofumaniwa Hotelini Mombasa,Kenya

Star wa bongo Hussein Machozi hatimaye amezungumzia tukio lililotokea mwezi uliopita na kupelekea vyombo vingi vya habari nchini Kenya kuripoti kuwa amekamatwa akizini na mke wa mwanasiasa maarufu mjini Mombasa, Kenya.
machozi-2

Haya ndio maelezo ya hit maker wa ‘Kwaajili Yako’ kuhusu kilichotokea, alipozungumza na Millard Ayo kupitia Amplifaya ya Clouds FM jana (Agosti 28).
“Ukweli ni kwamba hiyo story imekuzwa yaani imekuwa kubwa sana tofauti na jinsi mambo yalivyokuwa. Kama masaa 24 nilipewa sasa mbona bado nipo Kenya…Ile ishu ilikuwa hivi, tulikuwa tumekwenda kuingia deal hotelini kama tunavyokutanaga, sasa Yule mtu aliyekuwa ananipa deal alikuwa yupo pale hotelini akaniita twende tukaongee kupanga mikakati na kila kitu, lakini baadae kumbe alikuwa na beef sijui na mume wake au sio bana, kwahiyo mume wake alikuja pale kuanza kumletea fujo lakini mimi sikuwa kwenye uhusiano wowote, watu wakaleta fujo pale na nini mimi mbona nikaondoka fresh tu lakini hamna lolote ni kwamba tulikuwa tumekaa nae tunaongea mchakato wa biashara…hotelini kama maeneo ya kupumzika hivi kama sehemu ya mikutano hivi”.
Hussein Machozi afunguka jinsi alivyofumaniwa Hotelini Mombasa,Kenya Hussein Machozi afunguka jinsi alivyofumaniwa Hotelini Mombasa,Kenya Reviewed by CapchaMuzic on 06:21:00 Rating: 5
Powered by Blogger.