Hizi tuzo zingine kwa Rais Kikwete hapana
HABARI iliyosambazwa kwa vyombo vya habari ni kwamba Rais Jakaya Kikwete amepewa tuzo nyingine ya The Icon of Democracy. Ni icon au agony of democracy? Ajabu!
Pamoja
na wahusika kujisifu, ukichunguza sana unagundua kuwa nyuma ya tuzo hii
kuna Wanigeria. Kulikoni? Je, kuna matapeli wanaomzunguka Kikwete na
kusuka apewe upuuzi huu ili baadaye wahusika waje kumtumia baadaye kwa
kumtoa upepo au kutafuta fursa na kuchukua kwa njia za uwekezaji uchwara
kama ilivyokuwa kwenye tuzo nyingine ya kutia shaka ya The Most Impactful Leader of Africa iliyotolewa na Jarida lenye uhusiano na Wanigeria?
Kama Kikwete ni most impactful leader of Africa wale ambao ni truly most impactful watawekwa
fungu gani? Je, huu si utapeli wa mchana? Maana tunaambiwa yupo
Mwandishi wa habari ambaye pia ni pastor Elvis Ndubuisi Iruh kwenye tuzo
ya sasa sawa na African Leadership Magazine ambalo makao yake makuu ni 13 Mambilla street, Off Aso Drive, Asokoro.P. O. Box 9824 Garki – Abuja, Nigeria.
Je,
wahusika wanajua tabia ya Rais Kikwete ya kupenda sifa na kuthamini
sana waandishi wa nje kuliko wa ndani? Je, Kikwete na walioridhia
kupokea tuzo hii wanajua sifa za waliotoa tuzo husika?
Je,
mamlaka zetu, badala ya kupokea na kuwapatia tuzo, zinafanya utafiti na
kujiridhisha kuwa wanaotoa hizo tuzo wanafaa kufanya hivyo? Maana,
ukiangalia kinachoitwa tuzo na walioitoa unapata walakini.
Hata
jina la gazeti lenyewe shaka tupu ukiachia mbali mwenye kulimilki. Je,
kwanini wapokeaji hawakujiuliza maswali muhimu kuhusiana na tuzo husika
au ni kwa vile wanavishwa kilemba cha ukoko?
Je, kweli Kikwete ni Icon of Democracy (kielelezo cha demokrasia) au kinyume chake yaani Agony of Democracy? Hawa hawajafanya utafiti. Kama wameufanya, wamemhadaa.
Pia,
kutofanya utafiti ni ushahidi wa ukosefu wa uelewa wa wahusika. Ni
bahati mbaya, hata wanaopokea wanatenda kosa hilo hilo. Si kila
king’aacho ni dhahabu. Haiwezekani mtu aliyevuruga mchakato wa katiba
mpya ukiachia mbali kutuhumiwa kuingia madaraka kwa fedha iliyonyakuliwa
kwenye benki ya umma (EPA) asikanushe, akawa icon of democracy. Vinginevyo neno icon limepoteza maana kama si kumtapeli ili wahusika waje wamtumie baadaye.
Hata ukiangalia tuzo ya The most impactful leader haina
maana kwa mtu ambaye impact yake kwa uongozi na kutokaa ofisini
akitumia muda mwingi ughaibuni kwa shughuli ambazo zingeweza kufanywa na
waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Rais Kikwete anawezaje kuwa icon of democracy wakati
serikali yake inasifika kwa kutumia polisi kuwapiga hata kuwaua
wapinzani na waandishi wa habari na watetezi wa haki za makundi.
Rejea
mauaji ya watu watano kule Arusha kwenye mkutano wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mnamo Januari 2011, utesaji wa Dk.
Steven Ulimboka hapo Juni 26, 2012 na kutekwa na kuteswa kwa Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda hapo Machi 5, 2013, kutaja
kwa uchache bila kuongelea mauaji ya rejereja na mara kwa mara ya polisi
ya watu wasio na hatia katika sehemu mbalimbali nchini.
Kwanini
hawa kama si matapeli wa kawaida wa kinigeria, hawakuzingatia yote
haya? Tuzo za Kikwete ni kashfa kwa Watanzania hasa wahanga wa utawala
mbovu.
Rais
Kikwete hawezi kuwa the most impactful leader au icon of democracy kwa
madudu yote haya. Hapa hujaongelea ufisadi, uzembe, matumizi mabaya ya
fedha za umma na kutotimiza ahadi alizotoa kwenye uchaguzi wa
kidemokrasia. Hujaongelea uchakachuaji wa kura uliomwingiza madarakani
kwa kipindi cha pili. Hujaongelea mbinu chafu zilizotumiwa na kundi lao
la mtandao kuwachafua wenzake kwenye uchaguzi wa 2005 na matumizi mabaya
ya fedha na vyombo vya habari.
Cha
mno ni kutambua kuwa wanaompa nishani Rais Kikwete, licha ya kuwa
matapeli wa Kinigeria, wanajua fika kuwa wanachofanya ni kutumia upenyo
huo kuficha utapeli wao unaolenga kumtumia kwa sasa au baadaye
kujipatia nafasi kukamata rasilimali zetu.
Hebu
jiulize, yuko wapi yule profesa kidhabu aliyeandika kitabu cha Kikwete
kabla ya kugundulika kuwa kumbe ni kilaza anayedesa kazi za wenzake? Je,
ilikuwaje washauri wa Kikwete hawakungundua kuwa mtu kama huyu mwenye
usomi wa kutia shaka hakufaa kuandika kitabu cha Rais?
Hata
hivyo, utamlaumu nani wakati Rais mwenyewe anasifika kwa kuwakingia na
kuwateua watu waliotuhumiwa kughushi sifa za kitaaluma kama wale
waliotamalaki kwenye baraza lake la mawaziri na wengine ubalozini?
Je,
tumegeuka taifa la kitapeli au taifa la kutapeliwa kirahisi hata kwa
kusifiwa uongo na upuuzi? Je, waliomshauri Kikwete kupokea tuzo hizi
wanangoja nini ofisini iwapo itabainika watoa tuzo hizo si watu wa
kuaminika?
Chanzo: Tanzania Daima Agosti 20, 2014.
Hizi tuzo zingine kwa Rais Kikwete hapana
Reviewed by Unknown
on
12:02:00
Rating: