Hawa ndio Wachezaji 28 waliopitishwa Simba
MAJINA 28 ya wachezaji wa Simba waliosajiliwa
kwa ajili ya msimu ujao yalikabidhiwa juzi Jumanne katika kikao cha
Kamati ya Utendaji kilichoongozwa na Rais Evans Aveva ambachi
kilipitisha usajili huo.
Kabla ya kikao hicho, Kamati ya Usajili chini ya
Mwenyekiti Zacharia Hans Poppe na Makamu wake Kassim Dewji pamoja na
wajumbe wao, walikutana kujadili juu ya usajili wao huku beki mpya
aliyekuja kufanya majaribio, Butoyi Hussein, akipigwa chini.
Jana Jumatano saa 6 usiku ilikuwa ndio mwisho wa
usajili kwa klabu zote 14 za Ligi Kuu Bara ambapo Simba imepeleka majina
ya wachezaji 28.
Usajili wa Simba msimu ujao upo hivi; Makipa ni Ivo Mapunda na Hussein Shariff ‘Casillas’.
Mabeki ni Joseph Owino, Donald Mosoti, Abdi Banda,
Issah Rashid ‘Baba Ubaya’, Said Nassoro Masoud ‘Chollo’, Joram Mgeveke
na William Lucian ‘Gallas’,
Viungo ni Pierre Kwizera, Jonas Mkude, Shaban Kisiga, Said Ndemla, Amri Kiemba, Hassan Isihaka na Abdallah Seseme,
Washambuliaji ni Amissi Tambwe, Raphael Kiongera,
Haruni Chanongo, Awadh Juma, Uhuru Seleman, Elius Maguli, Ramadhan
Singano ‘Mess’ na Hussein Twaha Ibrahim.
Simba pia imepeleka majina manne ya usajili wa
wachezaji iliowaliowapandisha kutoka U-20 ambao wamefikisha idadi ya
wachezaji 28, hao ni kipa Manyika Peter, Mohamed Huseein ‘Tshabalala’,
Miraji Adam na Ibrahim Hajibu
Hawa ndio Wachezaji 28 waliopitishwa Simba
Reviewed by CapchaMuzic
on
00:53:00
Rating: