Breaking News: Bomu larushwa ndani ya basi Kigoma, watatu wauawa, sita wajeruhiwa

Kigoma. Watu watatu wamekufa akiwepo mtoto mchanga na wengine sita kujeruhiwa baada ya basi dogo la abiria (Hiace) kurushiwa bomu na watu wasiojulikana huko Kasesema, Kigoma alfajiri ya leo.
 AKithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Wilaya ya Buhigwe (OCD), Samwel Utonga alisema basi hilo lilikuwa likotokea Kilelema kwenda Kasulu Mjini ambapo watu hao walilirushia kitu kinachoaminika kuwa ni bomu.
Kamanda Utonga amesema majeruhi hao wamehamishiwa Hospitali ya Kasulu toka Hospitali ya Muyama baada ya hali zao kuwa mbaya.

Mwananchi
Breaking News: Bomu larushwa ndani ya basi Kigoma, watatu wauawa, sita wajeruhiwa Breaking News: Bomu larushwa ndani ya basi Kigoma, watatu wauawa, sita wajeruhiwa Reviewed by Unknown on 05:09:00 Rating: 5
Powered by Blogger.