TAARIFA KAMILI YA KIFO CHA MMILIKI NA MKURUGENZI WA SWEET FM NA SWEET TV, EMMANUEL MBUZA

Mmiliki
na mkurugenzi wa Sweet Fm radio ya mkoani Mbeya na Sweet Television,
Emmanuel Mbuza amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya
Tumbi alikokuwa akitibiwa baada ya kuugua kwa wiki mbili mfululizo.
Taarifa za uhakika toka kwa meneja wa Sweet fm, Yohana Mwambene
zinaeleza kuwa Mbuza ambaye pia alikuwa ni katibu mwenezi wa Chama Cha
Mapinduzi wilaya ya Mbeya mjini alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya
kisukari kilichompata ghafla pamoja na shinikizo la damu, magonjwa
yaiyomfanya awe na hali mbaya iliyopelekea kifo chake katika hospitali
ya Tumbi, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam alikokuwa amelazwa
kwaajili ya matibabu.
Emmanuel Mbuza (Mzaliwa wa mbeya aliyekua anafanya biashara zake jijini
Dar es salaam.) ni mhitimu wa
sangu High
school(2007), aliewahi kua Mfanyakazi wa Mbeya FM na generation FM, na
msomi wa Masters ya sheria aliyoichukua katika chuo kikuu cha Tumain cha
Iringa.
Mwili
wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kesho alhamisi kutokea jijini Dar
es Salaam kuelekea mkoani Mbeya ambako shughuli za mazishi zinatarajiwa
kufanyika katika makaburi ya ukoo maeneo ya kalobe jijini Mbeya, lakini
kwa sasa msiba Tabata jijini Dar es Salaam na Ilemi-Juhudi Mkoani Mbeya.
BWANA ametoa, BWANA ametwaa, jina lake lihimidiwe...AMEN
TAARIFA KAMILI YA KIFO CHA MMILIKI NA MKURUGENZI WA SWEET FM NA SWEET TV, EMMANUEL MBUZA
Reviewed by Unknown
on
08:23:00
Rating:
Reviewed by Unknown
on
08:23:00
Rating:
