HII INAWAHUSU WAREMBO WOTE IKIWEMO WEMA SEPETU, AUNT EZEKIEL, KAJALA, HAMISA NA WADADA WOTE TANZANIA
Moja kati ya urembo unaofanywa na wanawake wengi wa kisasa ni kuweka kope za bandia juu ya kope halisi, kweli wengi wanakuwa na mvuto wa aina yake wakikuangalia hasa mtoto wa kiume. Lakini hatari inayotokana na urembo huo ni kubwa zaidi ya matokeo ya muda mfupi. Wataalam wanaeleza kuwa kope za bandia ambazo hugundishwa kwa kutumia gundi ya nywele inayotumika kugundisha nywele bandia kwa wenye vipara inaweza kuwa chanzo cha upofu wa mtumiaji.
Gundi hiyo hupukutika taratibu sana kiasi cha kutoshtukiwa na kuelekea
kwenye mboni ya jicho ambayo ndio moyo wa ‘kuona’. Endapo mtumiaji
ataendelea kwa muda mrefu kutumia kope hizi bandia anaweza kujikuta
anakuwa na tatizo la kuona ama hata upofu wa haraka katika maisha yake
ya baadae. Hata hivyo, hatari kubwa imeelekezwa kwa maduka ama vibanda
vinatumia vifaa vya bei nafuu ikiwemo gundi inayotumika. Ukwepaji wa
gharama ama kutokuwa na uwezo wa kutumia gharama kubwa kunamuingiza
mrembo kwenye hatari zaidi. Kuwa mwangalifu, urembo usiwe chanzo cha
kuhatarisha afya yako. Kumbuka Afya ni uhai wa mwili wako.
HII INAWAHUSU WAREMBO WOTE IKIWEMO WEMA SEPETU, AUNT EZEKIEL, KAJALA, HAMISA NA WADADA WOTE TANZANIA
Reviewed by Unknown
on
04:39:00
Rating: