Diamond kuachia video za mbili kwa pamoja pia ijue sababu ya yeye kutopanda jukwaani baada ya Davido kuchukua tuzo ya BET,na kuhusu kutokwenda Wema Sepetu Marekani

Jumatatu Ijayo vituo vya runinga vya Afrika vitapokea video mbili mpya za mshindi wa tuzo 7 za KTMA Diamond Platnumz. Kama ambavyo Diamond tayari ameelezea mipango yake ya kutoa nyimbo mbili kwaajili ya masoko mawili tofauti, video moja ni kwaajili ya vituo vya nyumbani Tanzania na Afrika Mashariki, na ya pili ni kwaajili ya vituo vya Afrika magharibi.
diamond
Meneja wa Diamond, Babu Tale amesema video ya ‘Mdogo mdogo’ ambayo tayari audio imetoka itakuwa kwaajili ya TV za Tanzania na ‘Bum bum’ aliyomshirikisha Iyanya wa Nigeria itakuwa kwaajili ya TV za Afrika magharibi.
“Next week Monday tunaachia video mbili kwa wakati mmoja, tunaachia nyimbo ya mdogo mdogo kwa ajili ya African market especially East africa na Tanzania, tunaachia Bum Bum kwaajili ya west market”. Amesema Tale kupitia XXL ya Clouds FM leo.
Kuhusu kwanini Diamond hakupanda jukwaani baada ya Davido kushinda tuzo ya BET na kuwaomba nominees wenzake wa kipengele cha ‘Best Insternational Act: Africa’ ambacho Diamond alikuwa akiwania pia, wapande nae jukwaani, Tale ametoa sababu:
“Zile Tuzo zinarekodiwa before, diamond alikuwa anajua zile tuzo zinakwenda Live, sababu wote hawakuwa wameambiwa zinakwenda live au zinarekodiwa, wote wamelala kwenye hotel moja LA. Wakati wao wanamgongea Davido chumbani kwake alikuwa yuko tayari, Diamond alikuwa anajiandaa jioni ndo anakwenda kwenye hiyo show ya BET. Mwisho wa siku kwasababu wale walikuwa wanaenda na ratiba wakaona tutachelewa….hakujua kama inarekodiwa na wala hakujua kama Davido amechukua tuzo mpaka mimi ndio niliyemwambia”.

katika hali nyingine Watu wengi wakiwemo mashabiki wa Wema na Diamond walitarajia kumuona pamoja Wema Sepetu akimpa kampani mpenzi wake Diamond Platnumz ambaye alikuwa anawania tuzo ya BET Awards 2014 huko Los Angels, Marekani.
Wema alitarajiwa kuonekana kwenye red carpet ya BET kama ilivyokuwa kwenye MTV Africa Music awards ambapo walikuwa wote S.Afrika na kina Aunty Ezekiel na team ya Diamond
 Hata hivyo chanzo kimoja kilicho karibu na Wema na Aunty kimedai kuwa moja ya sababu iliyomfanya Wema ashindwe kwenda BET Awards licha ya kueleza kuwa angehudhuria kupitia Instagram siku kadhaa nyuma ni kufanyika kwa sherehe ya rafiki yao mmoja maeneo ya Mwananyamala nyumbani kwa Aunty Ezekiel juzi, ambapo asingeweza kuwaacha mashosti zake hao peke yao pasipo sapoti yake katika shughuli hiyo
Diamond kuachia video za mbili kwa pamoja pia ijue sababu ya yeye kutopanda jukwaani baada ya Davido kuchukua tuzo ya BET,na kuhusu kutokwenda Wema Sepetu Marekani Diamond kuachia video za mbili  kwa pamoja pia ijue sababu ya yeye kutopanda jukwaani baada ya Davido kuchukua tuzo ya BET,na kuhusu kutokwenda Wema Sepetu Marekani Reviewed by Unknown on 05:48:00 Rating: 5
Powered by Blogger.