VUNJA JUNGU KWA AUNT, WEMA NA KAJALA LIVE,WALA SAHANI MOJA WAKATA MAUNO YA KUFA MTU
Manguli wawili wa Bongo Movies waliokuwa mahasimu wakubwa Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na Kajala Masanja ‘K’ wakikata mauno.
Hatimaye!
Manguli wawili wa Bongo Movies waliokuwa mahasimu wakubwa na
kusababisha tafrani kubwa, Wema Isaac Sepetu ‘Beautful Onyinye’ na
Kajala Masanja ‘K’ hatimaye wamekutana uso kwa uso (live) na kumaliza
bifu lao saa chache kabla ya kuanza kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani,
NI KWENYE VUNJA JUNGU
Tukio
hilo la heshima lilijiri wikiendi iliyopita nyumbani kwa staa mwenzao
wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson, Mwananyamala jijini Dar
ambapo baadhi ya mastaa walikuwa wakivunja jungu katika sherehe ya
kumpongeza rafiki yao almaarufu kwa jina la Wise Ime aliyejifungua mtoto
wa kike hivi karibuni.
KWA MARA YA KWANZA TANGU WAGOMBANE
Katika tukio hilo, mastaa wenzao walipigwa na butwaa kuwaona wawili
hao wakiwa pamoja kwa mara ya kwanza tangu wagombane. miezi kadhaa
iliyopita.
WALA UJANA KAMA ZAMANI
Mastaa hao walinaswa pamoja wakiwa kama kumbikumbi wakila ujana kama
zamani, kitendo kilichowafurahisha marafiki zao wengine waliofika
nyumbani hapo wakimpongeza Aunt kwa kuwaweka pamoja kwani tangu
wapatanishwe hawakuwahi kukaa pamoja wala kula sahani moja kama
walivyofanya siku hiyo.
“Ukweli
sisi tumefurahishwa na ukaribu wa hawa mashosti tuliwamisi sana kuwaona
hasa kwenye shughuli kama hizi za kibao kata, leo wameshirikiana kama
zamani, wamezungumza, wamecheka na kukata mauno pamoja,” alisikika mmoja
wa mastaa aliyehudhuria katika shughuli hiyo.
MAUNO MWANZO-MWISHO
Kwenye shughuli hiyo kulipambwa na mauno mwanzo-mwisho yaliyoongozwa
na wapiga ngoma ya Kibao Kata ambapo kila mmoja aliinuka na kuonesha
ustadi wake wa kukata mauno.
HADI MAJOGOO
Shughuli hiyo iliendelea hadi majogoo kwani baada ya Kibao Kata,
mastaa hao walifunguliwa disko lililokuwa likiongozwa na madj maalum wa
Pro24djs huku MC akiwa ni Maimartha Jesse.
WEMA, KAJALA, AUNT WAPAGAWISHA
Katika shughuli hiyo, Wema, Kajala na Aunt walipagawishwa na wimbo wa
mpya wa mpenzi wa Wema, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ wa Mdogomdogo
ambapo waliingia kati na kuachia mauno hadharani.
Kuna
wakati Kajala na Wema waliachiwa nafasi ambapo walitoana jasho kwa
kukata mauno huku wakifuatisha vizuri wimbo huo utadhani walikuwa
wamefanya ‘riheso’.
ASANTE DJ
Baada ya kuserebuka kwa muda mrefu hadi wakatoka jasho, wawili hao
walisikika wakisema kuwa Dj alikuwa amewakuna mno kwani kila muziki
aliokuwa akiwawekea alikuwa akiwalenga na kuwafanya wachangamke zaidi
hadi shughuli ilipokwisha kila mtu akarudi kwake.
NENO LA WEMA
“Sasa hivi tupo vizuri sana. Yes tupo bega kwa bega ukizingatia ndiyo
tunaingia kwenye mwezi mtukufu. Nimefurahi sana kushea naiti na
Kajala,” alisema Wema.
NAYE KAJALA
“Kwani kuna tatizo? Hakuna tatizo. Sisi tupo vizuri kama alivyosema Wema tumeinjoi sana,” alifunguka Kajala.
TUMEFIKAJE HAPA
Miezi kadhaa Wema na Kajala waliingia kwenye gogoro kubwa na
kusababisha kuibuka kwa pande mbili za Team Wema na Team Kajala
zilizokuwa zinachochea ugomvi huku Kajala akitakiwa kurejesha zile Sh.
Milioni 13 alizolipiwa na Wema asiende jela miaka 7.
VUNJA JUNGU KWA AUNT, WEMA NA KAJALA LIVE,WALA SAHANI MOJA WAKATA MAUNO YA KUFA MTU
Reviewed by Unknown
on
10:17:00
Rating: