MOVIE YA FROLA MBASHA NA MUMEWE YAENDELEA, SASA WAZAZI WAINGILIA KATI.

Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili Bongo Flora Mbasha.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, kikao hicho kiliitishwa na baba wa Mbasha kwa kushirikiana na ndugu wengine wa pande zote mbili.
“Mbasha na mke wake, Flora walikutanishwa sehemu fulani jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupatanishwa. Kikao kilikuwa kizito, wakubwa wa familia zote walikuwepo lakini Flora alikataa mara tano kurudi kwenye ndoa yake.
UWAZI LAPIGA HODI NYUMBANI KWA MBASHA
Juzi Jumapili, Uwazi lilitia timu nyumbani kwa Mbasha, Tabata-Kimanga jijini Dar na kubahatika kuzungumza na baba na mama wa Mbasha bila kumpata Mbasha mwenyewe.
Mzee huyo aliyejitambulisha kwa jina la Maneno alikiri kuwepo kwa kikao kwa muda wa siku tatu tofauti lakini akasema mambo yalishindikana.
“Mimi nilikuja Dar kutokea Dodoma wiki moja iliyopita baada ya kupata wito wa mwanangu kuhusu mgogoro wa ndoa. Nilipofika hapa, sikumkuta Flora, nyumba ilikuwa tupu.
“Kikao kiliitishwa na pande zote mbili, akiwemo Mchungaji Gwajima ambaye alionekana kusuluhisha mgogoro wao lakini dalili za Flora hazikuonesha kuwa tayari kurudi kwenye ndoa yake,” alisema mzee huyo.
Emmanuel Mbasha.
KUNA MKONO WA MTU
Mzee Maneno aliendelea kusema: “Mimi kama mtu mzima, nilichokiona katika ndoa ya mwanangu kuna mkono wa mtu. Ila sasa ametumia mbinu kubwa sana kumrubuni Flora na yeye kakubali kurubunika.”
MAMA MZAZI NAYE
Kwa upande wake, mama mzazi wa Mbasha, Zulfa Maneno alisema kwake ni masikitiko makubwa kwa sababu mtoto wake alishakuwa na jina kubwa kimataifa na mkewe pia.
Alisema: “Mimi kwenye kikao nilipomwona Flora anakataa ndoa yake mara tano, kila akiulizwa anasema hataki kurudi mpaka mara tano, nikajua hakuna ndoa.
“Ninachojua, mgogoro huo wa ndoa ulitengenezwa kwa makusudi kabisa ili ndoa ivunjike. Ila kama aliamua kumwacha mwanangu angefanya hivyo kwa amani na si visa kama hivi.” 
Kuhusu kutakiwa shilingi milioni sitini ili Flora arejee kwenye ndoa yake, wazazi hao walisema hawajui kitu labda kama yanasemwa pembeni.
Baba mzazi wa Emmanuel Mbasha.
KULIKUWA NA MGOGORO Habari zaidi zinadai kwamba, fedha zinazotakiwa kulipwa ni kwa sababu, ndoa hiyo ilikumbwa na mgogoro kabla ya kuibuka kwa madai ya Mbasha kumbaka shemeji yake.
Flora aliwahi kufungukia hilo kwamba, kabla ya kutokea kwa madai ya ubakaji, alitibuana na Mbasha na akaamua kuondoka nyumbani kwenda kuishi hotelini. 
DALILI MBAYA
Kuna madai kwamba, siku ambayo Mbasha alikwenda kujisalimisha polisi (Juni 16, 2014), Flora alipigiwa simu kujulishwa lakini hakutokea kituoni.
Ikazidi kuelezwa kwamba, siku Mbasha anapelekwa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar kujibu madai ya ubakaji, pia Flora alijulishwa lakini hakutokea mahakamani hapo.
Mbali na kupelekwa mahakamani, habari za uhakika zinasema hata pale Mbasha alipokosa dhamana na kupelekwa kwenye Gereza la Keko, Flora alijulishwa, lakini hakufanya lolote.
“Je, kwa hayo yote ni kweli Flora anaipenda ndoa yake? Si jibu lipo wazi kwamba hakuna ndoa.” alisema mtu mmoja aliye karibu na familia hiyo.
Mama mzazi wa Emmanuel Mbasha.
MBASHA BAADA YA KUTOKA JELA
Ushahidi wa majirani umeweka bayana kwamba, Mbasha alipotoka gerezani na kufika nyumbani kwake, Tabata-Kimanga, Dar, walimfuata na kuangua kilio mbele yake huku wakimpa pole kwa mkasa mzima.
Baadhi ya majirani waliozungumza na Uwazi juzi, walisema kuwa siku hiyo nyumbani kwa Mbasha kulikuwa na dalili zote za kuwepo kwa msiba kwani vilio vilitawala.
MADAI
Mbasha, alipandishwa mahakamani Juni 17, mwaka huu kwa madai ya kumbaka mara mbili shemeji yake (jina tunalo).
Siku hiyo alikosa dhamana na kupelekwa Gereza la Keko ambapo Alhamisi ya Juni 19, mwaka huu alirudishwa tena mahakamani hapo kwa ajili ya dhamana. Kesi yake itaanza kusikilizwa Julai 17, mwaka huu huku ikielezwa kuwa upelelezi umekamilika. 
Kwa mahojiano kamili ya Mzee Maneno, mkewe na Uwazi fungua Global Tv Online kupitia.CREDIT:GPL
MOVIE YA FROLA MBASHA NA MUMEWE YAENDELEA, SASA WAZAZI WAINGILIA KATI. MOVIE YA FROLA MBASHA NA MUMEWE YAENDELEA, SASA WAZAZI WAINGILIA KATI. Reviewed by Unknown on 02:56:00 Rating: 5
Powered by Blogger.