HAYA NI ZAIDI YA MATESO:ugonjwa wa jicho unaomsumbua mtoto ambalo limefumuka na kutoka nje huku likitoa harufu kali na usaha
KWELI ni zaidi ya mateso! Ukisema we
unaumwa lakini unapata usingizi, kumbe hujawaona wagonjwa wenyewe!
Mtoto Neema Joseph (2) anateseka kwa ugonjwa wa jicho ambalo limefumuka
na kutoka nje huku likitoa harufu kali na maumivu yasiyo na mfano,
Mtoto Neema Joseph (2) akilia kutokana na maumivu makali ya jicho.
Mtoto huyo anayelia wakati wote
kutokana na maumivu, anaishi na mama yake mzazi, Annastazia Yohana (28)
kwenye Kijiji cha Bugomba, Kata ya Bulungwa wilayani Kahama, Shinyanga.
Akizungumza huku akimwaga machozi kwa
uzito wa tatizo la mwanaye, mama Neema alisema hali yake ya maisha
kiuchumi ni mbaya, hasa kufuatia kufiwa na mumewe, Josephat miezi tisa
baada ya kujifungua mtoto huyo huku akiwa analea watoto wenginewawili.
SIKIA KILIO CHA MAMA NEEMA
“Tangu mume wangu afariki dunia nimekuwa na maisha ya shida, sina msaada kwani hakuna ndugu wa mume wala wangu wenye hali nzuri ya maisha na walio tayari kunisaidia kubeba mzigo wa maisha yangu.
“Tangu mume wangu afariki dunia nimekuwa na maisha ya shida, sina msaada kwani hakuna ndugu wa mume wala wangu wenye hali nzuri ya maisha na walio tayari kunisaidia kubeba mzigo wa maisha yangu.
Annastazia Yohana Mama wa mtoto Neema akijitahidi kumbembeleza bila mafanikio.
“Hili tatizo la jicho la mwanangu
lilianza mwezi mmoja uliopita (Februari) ambapo lilianza kwa kuwa
jekundu huku likibubujika machozi mara kwa mara.
“Alikuwa akilifikicha kila wakati
kitendo kilichoniasharia kuwa mwanangu anapata mateso. Ndipo siku moja
nilimpeleka Kituo cha Afya cha Kata.
Walimchunguza na kumpatia matibabu, lakini hali ndiyo ilizidi kuwa mbaya,” alisema mama Neema.
Alisema jicho lilianza kutokeza kwa nje na kutoa mwonekano wa kutisha. Baadhi ya watu walimshauri ampeleke mtoto huyo kwenye Hospitali ya Nkinga.
Alisema jicho lilianza kutokeza kwa nje na kutoa mwonekano wa kutisha. Baadhi ya watu walimshauri ampeleke mtoto huyo kwenye Hospitali ya Nkinga.
“Nilipopata ushauri huo huku
nikioneshwa mmoja wa wanakijiji ambaye mwanae alitibiwa huko, nilimfuata
mama yangu mzazi na kumuomba aniangalizie wanangu wawili ambao mpaka
sasa anao.
“Niliuza chakula changu chote cha akiba ili kupata pesa ya nauli na matibabu,” alisema mama wa mtoto huyo.
“Niliuza chakula changu chote cha akiba ili kupata pesa ya nauli na matibabu,” alisema mama wa mtoto huyo.
HOSPITALI KUBWA NDIYO WANAWEZA
Mama Neema aliendelea kuweka wazi kwamba, madaktari wa Hospitali ya Nkinga walimfanyia uchunguzi mtoto wake na kusema tatizo lake linaweza kutibiwa Hospitali ya
Mama Neema aliendelea kuweka wazi kwamba, madaktari wa Hospitali ya Nkinga walimfanyia uchunguzi mtoto wake na kusema tatizo lake linaweza kutibiwa Hospitali ya
Kilimanjaro Christian Medical Center
(KCMC) iliyopo Moshi, mkoani Kilimanjaro. Alisema kwa kauli hiyo,
alilazimika kurejea nyumbani na mwanae kwa vile uwezo wa kufika huko
hakuwa nao.
ASAKA FEDHA, AENDA KUSAKA TIBA ZAIDI
Mama Neema aliendelea kusema: “Hali ya mtoto ikazidi kuwa mbaya zaidi. Sasa jicho lilizidi kutoka nje huku likiambatana na majimaji ya njano na harufu kali. Alikuwa akilia sana kwa maumivu.
Mama Neema aliendelea kusema: “Hali ya mtoto ikazidi kuwa mbaya zaidi. Sasa jicho lilizidi kutoka nje huku likiambatana na majimaji ya njano na harufu kali. Alikuwa akilia sana kwa maumivu.
“Ilibidi nisake fedha, nikampeleka
Kahama mjini kuomba msaada wa matibabu. Kule Kahama nilikutana na
wanawake watatu ambao walinieleza nifike uwanja wa michezo kuna
madaktari wa saratani walioletwa na Shirika la Huheso Foundation ambao
walinikabidhi kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama.”
MGANGA WA WILAYA AZUNGUMZA
Naye Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama, Helen Yesaya alikiri kumpokea mtoto huyo. Alisema alimpeleka kwa daktari wa macho ili kumfanyia uchunguzi zaidi wa kubaini kama tatizo la jicho hilo ni saratani au la!

“Hata hivyo, kwa vyovyote
itakavyokuwa ni budi mtoto huyu apelekwe Hospitali ya Rufaa ya Bugando,
Mwanza kwa ajili ya matibabu zaidi. Kama unavyomuona, jicho limeoza,
linatoa usaha, kwa kweli anahitaji kusaidiwa,” alisema Dokta Helen huku
akisikitika.
MAMA TENA
Akizungumzia taarifa hizo, mama wa mtoto huyo alisema hali yake kiuchumi ni mbaya, uwezo wa kuishi jijini Mwanza wakati mwanae akiendelea na matibabu hana, hivyo anawaomba Watanzania wamchangie fedha ambazo anaamini zitakuwa msaada wa kupata tiba bora ya mtoto wake.

KUTOA NI MOYO
Kwa yeyote aliyeguswa na tatizo la mtoto Neema anaweza kumsaidia kwa kuwasiliana na Shirika la Huheso Foundation la mjini Kahama kwa namba; 0753 444 840-Juma Mwesigwa, atawasiliana na mama Neema.
Kwa yeyote aliyeguswa na tatizo la mtoto Neema anaweza kumsaidia kwa kuwasiliana na Shirika la Huheso Foundation la mjini Kahama kwa namba; 0753 444 840-Juma Mwesigwa, atawasiliana na mama Neema.
HAYA NI ZAIDI YA MATESO:ugonjwa wa jicho unaomsumbua mtoto ambalo limefumuka na kutoka nje huku likitoa harufu kali na usaha
Reviewed by Unknown
on
02:08:00
Rating: